Joy FM
Joy FM
22 December 2025, 09:47

Jamii na wadau mbalimbali mkoani Kigoma wameaswa kujitokeza na kuwasaidia watoto yatima na wenye uhitaji ili nao waweze kujiona wanathaminiwa na jamii inayowazunguka.
Na Tresiphol Odace
Kituo cha tiba mbadala cha Lupimo Sanitarian Clinic kimetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima yanaolelewa katika kituo cha Subira Minal rahman kilichopo Kitongoni Manispaa ya Kigoma Ujiji ikiwa ni sehemu ya kituo hicho kurudisha fadhila kwa jamii.
Meneja Mkuu wa Lupimo Sanitarian Clinic Dkt. Emmanuel Madila amesema lengo la kutoa msaada huo ni kutaka kuoana watoto hao ambao wengi wao hawana baba wala mama wanajiona wakithaminiwa kama watu wengine huku akipongeza uongozi wa kituo hicho kwa namna ambavyo wameendelea kuwalea watoto na kuwapa madili mazuri.

Awali Mwenyekiti wa Kituo cha Subira Minal Rahaman Bi. Khadija Mpezi amekipongeza kituo cha Lupimo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine kuendelea kuwasaidia watoto huku Ust Abel Mukoko ambaye ni ustadhi wa madrasa ya Subira Minal Rahan akieleza namna wanavyohudumia watoto hao.
Hata hivyo, Kaimu Meneja wa Lupimo Sanitarian Clinic Aston Ngao amesema wametembelea kituo hicho na kuwapa msaada huo wa chakula siku ya sikuku za krismas na mwaka mpya.

Kituo cha Subira Minal Rahaman kinalea jumla ya watoto yatima na wanaoishikatika mazingira magumu 145 na vituo vilivyotolewa na kituo cha Lupimo Sanitarian Clinic ni pamoja na vyakula, mafuta, mikeka na vinywaji vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi laki saba na pesa taslim zaidi ya shilingi laki mbili.