Joy FM
Joy FM
19 December 2025, 15:33

Serikali imesema imedhamiria kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya usafirishaji kwa kujenga mpya mbili zitakazofanya kazi ziwa Tanganyika
Na Bukuru Daniel, Burundi
Tanzania imetenga shilingi bilioni 214 katika utekelezaji miradi ikiwemo ujenzi wa meli mpya mbili mkoani Kigoma ambazo zitasaidia katika kuchochea maendeleo ya nchi ikiwemo na ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumza katika mkutano wa Ujirani mwema ambao umefanyikia mkoani Burunga kusini mwa Burundi Mhe.Balozi Simon Sirro amebainisha kuwa mbali ya ujenzi wa meli hizo ambazo zitagharimu kiasi cha shilini bilioni 100 ,serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imejikita kuwekeza katika ujenzi wa barabara na anga ambavyo vimekuwa ni chachu ya maendeleo ya nchi.

Aidha amewataka wananchi kuitumia lugha ya kiswahili katika kukuza biashara katika ya Burundi na Tanzania kwani lugha hiyo imekuwa kiungo mhimu kinachowaunganisha raia wa nchi hizo na kusaidia katika mawasiliano katika utekelezaji wa shunguli mbali mbali zikiwemo maendeleo na ubadilishanaji wa biashara.
Balozi Simon Sirro ametoa wito wa kushirikiana kwa walinda usalama katika kukomesha vitendo vya uharifu ambavyo vimekuwa vikitoa hasa utekaji na uporaji katika ziwa Tanganyika unaofanywa na baadhi ya watu wenye nia mbaya ya kukwamisha maendeleo.

Mhe. Balozi Simon Sirro ametoa wito wa kuheshimiwa kwa mipaka na kufuata sheria kutokana na kuongezeka kwa wimbi la wakimbizi kutoka DRC wanaoikimbia nchi yao kutokana mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi katika ya vikosi vya serikali na kundi la waasi la M23.