Joy FM
Joy FM
19 December 2025, 14:09

Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo inatajwa kuchochea uchumi na kipato kupitia mapato yatokanayo na miradi hiyo
Na Lucas Hoha
Manispaa ya Kigoma Ujiji inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa mwaka kutoka chanzo cha mapato cha soko la mwanga linaloendelea kujengwa tofauti na awali ambapo Manispaa ilikuwa ikikusanya shilingi milioni 4 kwa mwaka
Akizungumza na waandishi wa habari wakati mara baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Serikali, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Kisena Mabuba amesema serikali imedhamiria kufungua Mkoa wa Kigoma kiuchumi kwa kutekeleza miradi ya kimkakati.
Amesema kutokana na uwepo wa soko la Mwanga na miradi mingine itasaidia manispaa kujiendesha kutokana na ukusanyaji wa mapato.

Aidha ameongeza wakati soko hilo linavunjwa wapo wafanyabiashara waliohamishwa hivyo ujenzi wa soko utakapokamilika watapewa kipaumbele wale ambao walikuwepo awali ili kuondoa migogoro.
Akizungumzia soko hilo, Mkandarasi mjenzi wa soko la Mwanga amesema ujenzi wa soko hilo umefikia asilimia 43 nakuwa wamechelewa kukamilisha mradi huo kutokana na mvua zilizonyesha mfululizo nakuwa ifikapo mapema mwaka 2026 wanakamilisha mradi huo.