Joy FM

Wachungaji watakiwa kuwa kielelezo cha kulinda maadili Kigoma

9 December 2025, 12:32

Katibu tawala Wilaya Kigoma mwenye suti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja na wachungaji waliotimu mafunzo, Picha na Prisca Kizeba

Katibu tawala Wilaya Kigoma Mganwa Nzota amesema wachungaji wana wajibu wa kuhakikisha wanalinda na kukemea maadili kwenye jamii ili kuwa na kizazi chenye maadili mema

Na Prisca Kizeba

Wachungaji Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuwa kielelezo katika kulinda mmonyoka wa maadili katika jamii

Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala Wilaya Kigoma Mganwa Nzota wakati akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kigoma katika mahafali ya wachungaji wa chuo cha Edin Mition kilichopo manispaa ya kigoma ambapo amesema wachungaji wanao wajibu wa kusaidia jamii katika kulinda mmomonyoko wa madili katika jamii.

Sauti na Katibu tawala Wilaya Kigoma Mganwa Nzota

Mganwa ameongeza  kuwa viongozi wa ndini ndio kiini cha kulinda amani na kuwa hawana budi kuhamasisha waumini kuendele kulinda amani.

Sauti na Katibu tawala Wilaya Kigoma Mganwa Nzota

Naye Mkurugenzi wa chuo hicho Kenneth Rwego Gahuriro amesma lengo la kuwafundisha wachungaji kuwapa uwezo wa kuendelea kupambanua mambo ya kiroho na kijamii kwa ujumla.

Sauti ya Mkurugenzi wa chuo hicho Kenneth Rwego Gahuriro

 Nao baadhi ya wachungaji waliohitimu mafunzo hayo wameeleza umuhimu wa elimu walioipata.

Sauti ya baadhi ya wachungaji