Joy FM

Wazazi, walezi watakiwa kuwajengea misingi ya maadili watoto Kigoma

9 December 2025, 10:03

Baadhi ya watoto wa Kanisa la MMPT Kikunku  Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Sofia Cosmas

Katika jamii yoyote yenye matumaini ya kupata viongozi bora, jukumu la malezi ya watoto ni la msingi na la lazima na mojawapo ya nguzo muhimu zinazoweza kuwaongoza watoto kuwa viongozi wenye maadili ni kuwajengea msingi imara wa imani ya kimungu.

Na Sofia Cosmas

Wazazi na walezi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameaswa kuwajengea watoto msingi wa imani ya kimungu ili kuwapata viongozi wenye maadili ya kimungu.

Ni baadhi ya watoto wakisoma vifungu vya maandiko  katika biblia wakati wa sherehe ya watoto  iliyoambatana na maadhimisho ya  kuzaliwa  kwa Bwana Yesu katika kanisa la MMPT Kikunku  Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mgeni rasmi katika sherehe hiyo  alikuwa Mwnjilisti Boniphasi Emmanueli amewataka wazazi na walezi kuwajengea watoto msingi wa kimungu ili wakue katika maadili ya Kimungu.

Aidha ili kuhakikisha watoto wanapata mafundisho katika mazigira safi na salama amechangia mifuko kumi ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa  darasa la watoto.

Baadhi ya watoto wa Kanisa la MMPT Kikunku  Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Sofia Cosmas

Awali katika  risala kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Mwalimu Erasto Isaya Takato ameeleza malengo ya kuanzishwa kwa  umoja wa  watoto katika kanisa la MMPT kikunku   ni kuwalea watoto kimungu na kuwafanya kuwa jasiri katika kumtumikia Mungu.

Kwa upande wao watoto wa kanisa hilo wameeleza namna ambavyo darasa hilo limewanufaisha kwa kuwafundisha  kumjua Mungu na malezi bora.

Umoja huo wa watoto ktika kanisa ka MMPT Kikunku (CYM) ulianzishwa mwaka 1996 chini ya waasisi marehemu Mwal.  Isaya Takato na Mwl. Wiliamu Stephano ambaye kwasasa dio askofu wa kanisa la MMPT misheni ya Gungu na walianza na watoto 8 na mpaka sasa wana watoto zaidi  100 wanaohudhuria mafundisho.