Joy FM
Joy FM
8 December 2025, 16:23

Wito umetolewa kwa jamii kuendelea kukemea vitendo vya ukatilii ambavyo vimekuwa vikifanyika kwa jamii
Na Prisca Kizeba
Wanawake Katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameaswa kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili unaoendela katika jamii
Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi wa jamii Exavery Nkyami wakati wa maombi kumshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka salama kwa wanawake wa kanisala TAG ambapo amesema kila mwanamke anawajibu wa kulinda mtoto wake ili kuhakikisha mtoto hafanyiwi ukatili
Naye Mwangalizi wa section hiyo Dkt. Galishoni amesema wanawake wanao wajibu wa kutunza ndoa zao ili kuwa na utumishi bora katika jamii na kanisa kwa ujumla
Sambamba na hayo, Wanawake hao wamehitimisha kwa kutembelea wafungwa katika gereza la Bngwe na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa wa gereza la Bangwe.

Akipokea zawadi hizo Mkaguzi Msaidizi wa magereza afande Arnold ametoa shukrani na kuwaasa kuendelea kuwa na moyo huohuo ili kuwa mabalozi kwa watu wengine
Nayea mwenyekiti wawanawake Liliani Magesa amesema kuwa kila mtu anao wajibu wakujitoa kuwasadia watu wengine waliopo kwenye matazizo ili kuwa na utumishi ulio kamilika
Baadhi ya wanawake waliohudhuria maombi hayo wamekuwa na haya yakueleza kuhusu ukatili