Joy FM
Joy FM
5 December 2025, 09:05

Mkuu wa Wilaya Uvinza Mkoani Kigoma Dinah Mathamani amesema wataendelea kufanya oparesheni ili kubaini na kukamata nyavu haramu zinazotumiwa na wavuvi ndani ya ziwa Tanganyika
Na Mwandishi wetu
Serikali wilayani Uvinza imeziteketeza nyavu haramu 197 katika Kijiji cha Rubengela kata ya Sunuka Leo tarehe 4 Desemba,2025 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika.

Zoezi hilo limefanyika chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh. Dinah Mathamani, ambaye aliongoza viongozi na maafisa uvuvi katika kuhakikisha nyavu hizo hazirejei tena kwenye matumizi.

Mh. Mathamani amesisitiza kuwa serikali haitavumilia mtu yoyote anayejihusisha na uvuvi haramu, kwa kuwa vitendo hivyo vinaharibu mazalia ya samaki na kuhatarisha uchumi wa wavuvi wanaofuata sheria. Ameeleza kuwa oparesheni za kukamata na kuteketeza zana haramu ni endelevu na zitafanyika katika maeneo yote ya Wilaya Uvinza.
Aidha, wananchi wa Rubengela wamepongeza serikali kwa kuchukua hatua hiyo, wakisema kuwa uvuvi haramu umekuwa ukipunguza sana upatikanaji wa samaki na kuathiri mapato ya kaya.
