Joy FM

Walia na mkandarasi kuelekeza maji kwenye nyumba zao Kigoma

4 December 2025, 17:44

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua akizungumza na wananchi ambao nyumba zao zinapitiwa maji, Picha na Lucaa Hoha

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dk. Rashid Chuachua ameagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa Bangwe – Ujiji kuhakikisha anajenga mitaro ya kupitisha maji ambayo yamekuwa yakiathiri wananchi.

Na Lucas Hoha

Baadhi ya wananchi wa kata ya Bangwe maeneo ya Magela Manispaa ya Kigoma Ujiji wamelalamikia mkandarasi anayejenga barabara kutoka Bangwe kwenda Ujiji kuelekeza mitaro ya maji kwenye makazi ya watu jambo ambalo linahatarisha usalama wa nyumba zao.

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt.Rashid Chuachua akitoa maelekezo wakati akizungumza na wananchi wa Bangwe, Picha na Lucas Hoha

Wakizungumza na Radio joy FM baadhi ya wananchi hao wamesema awali wakati ujenzi huo unaanza walitoa ushauri kwa mkandarasi wa mradi kuhusu mitaro ya maji lakini hakufuata ushauri na Sasa maji yanayotokana na mitaro imekuwa kero kwa wananchi

Kutokana na malalamiko hayo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashird Chuachua amefika eneo la tukio kuona hali halisi ya athari inayotokana na maji hayo

Amesema wananchi hao wako kwenye hatari ya nyumba zao kubomoka nakuagiza mkandarasi wa mradi kukaa kikao cha kutafuta fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji hayo ili wananchi wawe salama.