Joy FM

Madiwani watakiwa kuwatumikia wananchi Kasulu

4 December 2025, 14:36

Mwenyekiti wa halmashauri aliyechaguliwa na madiwani Bw, Samwel Filberty kadogo pamoja na makamu wake Bw, Charles Benjamin, Picha na Emmanuel Kamangu

Katibu tawala Mkoa wa Kigoma amewataka madiwani katika Halmashauri ya Wilaya Kasulu kuhakikisha wanawatumikia wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao

Na Emmanuel Kamangu

Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kusimamia vyema shuguli za maendeleo kwa wananchi wao.

Amebainisha hayo, Mwakilishi wa Katibu tawala mkoa wa kigoma Bw. Patrick Kigere akiwa katika mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya kasulu mkutano ambao umebebwa na agenda  kuu    ya kuapishwa kwa madiwani, kumchagua mwenyekiti wa halmashauri na makamu wake ikiwa ni pamoja na kuunda kamati mbali mbali za kudumu za halmashauri ambapo ametumia mwanya huo kuwataka madiwani kufanya kazi kwa juhudi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya kasulu Bi, Teresia Mtewele amewasihi madiwani kukaa karibu na wananchi wao ikiwa ni kujua kero zinazowakabili  na kuzishugulikia kwa wakati.

Madiwan halmashauri ya wilaya kasulu mara baada ya kupata kiapo, Picha na Emmanuel Kamangu

Aidha mwenyekiti wa halmashauri aliyechaguliwa Bw, Samweli Kadogo pamoja na makamu wake Bw, Charles Benjamini wamesisitiza umoja ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

Naye mbunge wa jimbo la kasulu Vijijini Bw, Edibil kazala akiwa ni sehemu ya baraza la madiwani  wa halmashauri ya wilaya ya kasulu amewataka madiwani kuwatumia wananchi kikamilifu na kuwa tayari kutatua kero zinazowakabili.