Joy FM
Joy FM
2 December 2025, 11:52

Madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkaoni Kigoma wametakiwa kuhakikisha wanafuatilia na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao
Na Mwandishi wetu
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Elisante Mbwilo amewataka waheshimiwa madiwani kuwatumikia wananchi kwa uaminifu na uadilifu kama walivyoapa kwenye kiapo chao
Ameyasema hayo leo Desemba 02, 2025 alipokuwa akihutubia Mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani Manispaa ya Kigoma Ujiji uliofanyika katika ukumbi wa NNSF Kigoma mara baada ya badiwani wateule kula kiapo cha utii na ahadi ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma.

Aidha amewataka kusimamia vyema miradi ya maendeleo sambamba na ukusanyaji wa mapato kikamilifu na kuhakikisha Wananchi wanapata maendeleo.
