Joy FM
Joy FM
24 November 2025, 12:32

Wazazi na Walezi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wametakiwa kuwa na desturi ya kuanda lishe bora kwa watoto
Na Dotto Josephati
Wazazi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wanatakiwa kuongeza juhudi kwa kuwachangia chakula cha watoto wao shuleni ili iwasaidie kuongeza ufanisi wa kujifunza wanapokuwa katika masomo yao.

Wito huo umetolewa na Afisa Mtendaji wa kata ya Kitahana Bw. Fundi Hamisi katika Kijiji cha Rugunga Kata ya Kitahana katika kilelecha maadhimisho ya siku ya lishe ambapo amesema upatikanaji wa chakula kwa watoto shuleni utawasaidia kujifunza katika mazingira mazuri pindi wanapokua shuleni.
Naye afisa elimu Kata Bi. Zuwena Yusufu amesema watoto wanapopata chakula shuleni inawaidia kufanya vizuri katika masomo huku Afisa kilimo Bw. Rajabu Ridhiwa akiwahimiza wananchi kujenga tabia ya kulima mbogamboga na matunda angalau eneo dogo majumbani mwao ili iwasaidie kuboresha afya zao.
Kwa upande wake, Afisa lishe Wilaya ya Kibondo Bi. Jakline Sospita amewataka wazazi kuzingatia mlo kamili wanapokuwa wanaandaa chakula cha watoto wao ili wakue katika hali njema.