Joy FM
Joy FM
22 November 2025, 11:17

Licha ya mikakati inayoendelea kuweka na Serikali ya Burundi ya kuhakikisha inasaidia kuondoa watoto wanaoishi mitaani bado watoto hao wameendelea kuonekana namitaani na wengine wakijikuta katika kazi zisizo rasmi
Na Bukuru Daniel
Mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi Bujumbura unaendelea kushuhudia ongezeko la watoto wanaoishi mitaani, licha ya wito wa mara kwa mara kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu na hatua zinazoendelea za serikali.
Wengi wa watoto hao ambao wengi wao ni chini ya umri wa miaka 18, walisema walihama kutoka vijijini kati ya Aprili na Juni mwaka huu kwa ajili ya kutafuta maisha bora. Wanaishi katika maeneo ya kawaida ya mijini, haswa masoko. Wengine huuza bidhaa ndogo ndogo wakati wengine wanafanya kazi kama wabeba mizigo.
Huku wengine wakilala kwenye mitaro ya kupitishia maji kwenye
barabara kuu, wakaazi wanasema uhalifu wa mitaani hasa uporaji wa mabegi na simu nyakati za jioni unaongezeka.
Mapema wiki hii, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani na usalama Pierre Nkurikiye alionyesha wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa idadi ya watoto wa mitaani, wanaoacha shule, na mimba za mapema maswala ambayo alihusisha na ufadhili duni wa muda mrefu.
Idadi ya watoto wa mitaani imefikia karibu 7,000 na zaidi ya watoto 260,000 wanaacha shule kila mwaka.
Alikosoa bajeti ndogo inayotolewa kwa mipango ya ulinzi wa watoto.Mashirika ya kiraia pia yalionyesha wasiwasi.Shirika la kitaifa la kupambana na uhalifu wa kimataifa (ONLCT), shirika mashuhuri la kutetea haki za watoto, lililaani ongezeko la idadi hiyo na kutaja changamoto zaidi, ikiwa ni pamoja na watoto ambao hawajasajiliwa katika ofisi ya usajili wa kiraia kuwafanya wawe katika hatari ya kuambukizwa magonjwa.
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Burundi imejaribu kuzuia ongezeko la watoto wa mitaani. Tangu mwaka wa 2024, polisi wamefanya oparesheni za mara kwa mara za kuwatafuta na kuwakamata, wakikusanya zaidi ya watoto 300 na kuwapeleka katika vituo vya kurekebisha tabia, kikiwemo kimoja cha Mishiha, jimbo la Cankuzo.
Licha ya hatua hizi, watoto wengi hatimaye hurudi mitaani. Waliohojiwa walitaja hali ngumu katika vituo hivyo kuwa ni pamoja na uhaba wa chakula.