Joy FM
Joy FM
20 November 2025, 11:32

Viongozi wametakiwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na uwajibikaji
Na Hagai Ruyagila
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta amewahimiza viongozi wa Dini na watumishi wa umma nchini kuwatumikia wananchi kwa nidhamu, uadilifu, uwazi na uwajibikaji ili kuendeleza misingi bora ya kuaminika katika jamii.
Akizungumza na waumini wa kanisa la Anglikana Kanda ya Kasulu Mjini, Askofu Bwatta amesema utumishi mzuri ni kiongozi kutumia nafasi yake kwa nidhamu na uadilifu vitu ambavyo ni nguzo muhimu katika kujenga utumishi bora unaoaminika, nakuwa manufaa kwa jamii anayoiongoza.
Mkurugenzi wa Kanisa la Anglikana Kanda ya Kasulu Mjini, Canon James Bigombo amewasihi waumini wa dini ya Kikristo kuendelea kuliombea taifa ili amani iendelee kutamalaki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kanisa la Anglikana Kanda ya Manyovu, Canon Yohana Nyoka amewahimiza waumini wa dini ya Kikristo kumtumikia Mungu kwa uaminifu katika maisha yao.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo wamesisitiza umuhimu wa viongozi wote kuwa na maadili na moyo wa utumishi.