Joy FM

DC Kasulu ataka watumishi wa umma kuanzisha mashamba darasa

19 November 2025, 12:33

Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akiwa wakulima na watumishi wa umma wakati akigawa miche ya Kahawa, Picha na Hagai Ruyagila

Mashamba darasa ni maeneo maalumu yanayotumika kufundishia na kuonesha mbinu mbalimbali za kilimo kwa vitendo na ni darasa wazi linalomuwezesha mkulima kujifunza kwa kuona na kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kilimo.

Na Michael Mpunije

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu amewataka watumishi wa umma katika Halmashauri ya Mji Kasulu kuanzisha mashamba darasa ya kilimo cha mazao ya biashara ili kutoa hamasa kwa wananchi kulima mazao hayo.

Kanali Mwakisu ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa umma katika halmashauri ya mji Kasulu na kueleza kuwa Serikali imekuwa ikitoa wataalamu wa kilimo kwa ajili ya kuwafikia wakulima na kutoa elimu ya kulima mazao ya Biashara ambayo huwasaidia kuinua uchumi wa Kulima.

Amesema kila mtumishi wa umma anatakiwa kulima angalau ekari moja katika mazao ya kimkakati ikiwemo zao la Kahawa,mchikichi na Pamba ili kutoa hamasa kwa wakulima wengine kuchangamkia fursa hizo.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isaac Mwakisu

Insert01…..DC mwakisu watumishi

Baadhi ya watumishi wa umma katika halmashauri ya mji Kasulu wamesema wameshaanza mchakato wa kutafta maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo lengo ikiwa ni kutoa motisha kwa wananchi kuona umuhimu wa kilimo cha mazao ya Biashara kwa ajili ya kukuza uchumi wao.