Joy FM
Joy FM
18 November 2025, 11:50

Serikali ya Mkoa wa Kigoma imewatoa shukrani kwa wawakilishi wa nchi na wadau wa maendeleo kwa kufanikisha kuendelea kufadhili miradi mbalimbali ya kijamii katika kambi za wakimbizi zilizopo Kigoma
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amekutana na mabalozi na wawakilishi kutoka kwenye balozi za nchi wadau wa Maendeleo, ambao wamewasili mkoani hapa leo Novemba 18, 2025 kwa ajili ya kutembelea Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu na Nduta wilayani Kibondo ili kujionea Shughuli zinazofanywa na Mashirika mbalimbali ya kuhudumia wakimbizi mkoani hapa.

Kupita Mazungumzo yao, Balozi Sirro ameyashukuru mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohudumia wakimbizi kutoka nchini Burundi na Congo DR, yaliyopo katika Mkoa wa Kigoma sambamba na uwezeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii kwa wakazi wanaokaa katika maeneo yanayozunguuka kambi hizo unaoratibiwa na kutekelezwa na Program ya Pamoja ya Kigoma (KJP).
Aidha, ameueleza ujumbe huo kuwa, wakimbizi kutoka nchini Burundi wapo katika hatua ya kurejea kwao kutokana na hali ya amani na utulivu kutengemaa nchini humo.
