Joy FM

Wahitimu VETA Kibondo wahimizwa kujikwamua kimaisha

17 November 2025, 17:12

Wahitimu katika chuo cha ufundi stadi veta Wilayani Kibondo mkoani Kigoma wamehimizwa kutumia mafunzo waliyoyapata kwa ajili ya manufaa yao ili waweze kujikwamua katika maisha yao ya kila siku hali itakayopunguza wimbi la vijana wasio na ajira hapa nchini.

Na Dotto Josephati

Wito huo umetolewa na Afisa elimu ya watu wazima kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo katika mahafali ya 58 ya chuo hicho Bw. Filbert Misuzi ambapo amewataka wahitimu kwenda kutumia taaluma zao kwaajili ya kujikwamua kiuchumi na kuachana na makundi yasiyofaa ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao

Bw. Filbert Misuz ~Afisa Elimu ya watu wazima

Naye Mkuu wa chuo hicho Bw. Robert Kihwele amewaasa wahitimu kuwa tayari kujifunza kwa yale watakayo kutana nayo katika maeneo yao ya kazi ili waendelee kujiongezea ujuzi na utaalamu zaidi katika kazi zao.

Bw. Robert Kihwele ~Mkuu wa chuo

Wahitimu katika risala yao mbali na kueleza mafanikio waliyoyapata wakati wote walipokua chuoni hapo wamemuomba mgeni rasmi kuwatatua changamoto zinazo wakabili ndani ya chuo hicho ili waweze kujifunza Kwa ufanisi zaidi Katika masomo yao.

Wanachuo