Joy FM
Joy FM
13 October 2025, 10:55

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kitaendelea kuwatetea wananchi wa Kigoma hususani wenye changamoto ya kupata vitambulisho vya uraia, kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa na kuufanya mji wa Kigoma kuwa wa kimkakati
Na Mwandishi wetu
Mgombea ubunge katika Jimbola Kigoma Mjini Kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema atahakikisha anaufanya mji wa Kigoma kuwa kituo cha biashara na kuchochea ajira kwa wananchi na kuwa na uwezo wa kutoa mikopo kwa makundi mbalimbali ya vijana na akina mama.
Akizungumza katika Mkutano wa kampeni katika uwanja wa Mwanga Communty Centre amesema dhamira yake ni kuhakikisha anakuza uchumi wa wananchi kupitia shughuli mbalimbalimbali za uchumi kwa kuanzisha na kuendeleza miradi ya kiuchumi.

Aidha amesema ataendelea kupigania wananchi wa Kigoma ili waweze kupata haki ya uraia ili wasiendelee kusumbuliwa na suala la kukosa vitembulisho vya uraia.
“nitaendelea kuwatetea watu wa mipaka mingine hawasumbuliwi uraia, watu wa Arusha hawasumbuliwi uraia, watu Malawi hawasumbuliwi uraia sasa kwanini watu wa Kigoma tuendelee kusumbuliwa uraia nitahakikisha hamsumbuliwi tena”
Zitto Kabwe amesema kuwa lengo la chama hicho ni kuandaa mpango kabambe wa kuifanya miji ya Bangwe na Kagera kuwa Satellite town ili iendelee kuwa ya kuvutia kutokana na ongezeko la watu wanaoendelea kujenga na kupanua mji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ngome ya vijana Taifa wa chama cha ACT Wazalendo, Abdull Nondo amesema kuwa chama hicho kina viongozi mahili wa kutetea wananchi na kuwaletea maendeleo.
Baadhi ya wagombea ubenge kutoka majimbo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma wamewataka wananchi kuhakikisha wanamchagua zitto Kabwe ili aweze kurudisha heshima ya Kigoma kwenye siasa na kuwatetea wananchi kwa kutatua changamoto zao ikiwemo afya, elimu, miundombinu ya barabara na kuufungua Mkoa wa Kigoma