Joy FM

Mgombea ubunge CUF aahidi pembejeo za kilimo na kusaidia wavuvi Kigoma

11 October 2025, 11:56

Mgombe ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini Kashindi Ally akizungumza na wanachama na wananchi wa kata ya Mwandiga Kigoma, Picha na Tryphone Odace

Chama cha CUF kimesema kitaendelea kusimamia haki za wananchi ikiwemo kutatua changamoto zinazowakabili hasa miundombinu ya barabara za mitaa, afya na huduma zote za kijamii

Na Mwandiahi wetu

Mgombe Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha CUF Kashindi Ally amesema miongoni mwa vipaumbele vyake atakavyoanza iwapo atpew ridha ya kuongoza Jimbo hili ni pamoja na kushughulikia zinawakabili wavuvi, afya na suala pembejeo za kilimo kwa wakulima.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika kata ya Mwandiga, Bw. Kashindi Ally amesema kuwa suala la mbolea na pembejeo zimekuwa kikwazo kwa wakulima kwani zinawafikia wakulima zikiwa zimechelewa na kusababisha kukosa mazao yenye tija.

Wananchi na wanachama wa CUF wakiwapokea viongozi wao wakiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya mwandiga, Picha na Tryphone Odace

“mimi nimezaliwa hapa mwandiga na nimefanya kazi muda mrefu za kilimo na tumekuwa tukilima na kukosa pembejeo kwani zinakuja zimechelewa na kusababisha tukose mazao yenye uhakika aubwakati mwingine kukosa na kubaki na njaa lakini nimekuja kuwa mkombozi wenu kwenye kilimo nitashughulikia suala la mbolea na pembejeo zote ili ziweze kuwafikia mapema”

Amesema kuwa atahakikisha pia anatatua changamoto zinazowakabili wavuvi zinatatuliwa ili waweze kufanya shughuli zao bila kikwazo chochote.

“mimi nitahakikisha nawasaidia wavuvi ili waweze kuendelea na shughuli zao za uvuvi maana huwezi kusema unafunga ziwa wakati hujui nyakati na majira ya kuvua ziwa linajifunga lenyewe halihitaji degree wala diploma kulifunga sasa nitahakikisha ziwa halifingwi ili muendelee kuvua na kupata kipato”

Mwenyekiti wa chama cha CUF Mkoa wa Kigoma Yasin Mambobado amesema kuwa mgombea wao anasimamia na kuleta maendeleo kwa wananchi huku mgombea udiwa wa kata ya mwandiga akiahidi kuboreha barabara zote za mitaani.

Wananchi na wanachama wa CUF wakiwapokea viongozi wao wakiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya mwandiga, Picha na Tryphone Odace

Kwa upande wake, Mjumbe wa baraza kuu la uongozi Taifa ambaye pia ni Mgombea udiwani kata ya Mwndiga Mamisho Ruyange amewataka wananchi kutokubali kupokea rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.

Kampeni zinendelea nchini kwa wagombea kunadi sera zao kwa wananchi ikiwa ni siku chache zimesalia kuelekea siku ya kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika mwezi huu wa kumi tarehe 29 mwaka 2025.