Joy FM
Joy FM
22 September 2025, 12:23

Wafugaji na wakulima wameomba Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuendeleaa kuwapa mikopo ili waweze kuendesha shughuli zao na kuongeza thamani ya bidhaa wanazozalisha
Na Tryphone Odace
Benki ya Kilimo Tanzania TADB imesema inaendelea kufanya mapinduzi ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima na wafugaji ili waweze kutoka kwenye kilimo cha kujimu na kufanya kilimo biashara ili kuongeza thamani ya mazao na uzalishaji wenye tija.
Afisa biashara kutoka Benki ya kilimo Tanzania Patrick Kafungu amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda cha Mayai Limited kilichopo kijiji cha Kaseke halmashauri ya Wilaya Kigoma ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa mayai baada ya kupata uwezeshaji kutoka benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania.
Bw. Kafungu amesema lengo ni kuhakikisha wanawasaidia wakulima wadogo wadogo na wafugaji ili waweze kuongeze thamani mazao yao ambapo kiwanda hicho kwa sasa kinaweza kuzalisha kreti za mayai ya kutosha jambo ambalo linatajwa kuwanufaisha.
Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Mayai Limited, Bw. Lupinda Sing Sundru amesema benki ya kilimo Tanzania TADB imeweza kuwapa asilimia 80 ya uwezeshaji na hivyo kuwainua na kuongeza uzalishaji kiwandani hapo.
Aidha ameongeza kuwa mradi huo mpaka sasa una kuku elfu tisini na mbili na kuwa na uwezo kuzalisha kreti za mayai 3000 kwa siku na unatajwa kuongeza ajira kwa wananchi hasa wanaozunguka mradi huo.
Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Mayai Limited Lupinda Sing Sundru amesema benki ya kilimo tanzania TADB imeweza kuwaoa asilimia 80 ya uwezeshaji na hivyo kuwainua na kuongeza uzalishaji.
Aidha ameongeza kuwa mradi huo mpaka sasa una kuku elfu tisini na mbili na kuwa na uwezo kuzalisha kreti za mayai 3000 kwa siku na unatajwa kuongeza ajira kwa wananchi hasa wanaozunguka mradi huo.

Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wameeleza namna wanavyofaika na kiwanda hicho na kuwa wameweza kuendesha maisha ya familia zao.