Joy FM

Madereva bodaboda watakiwa kufuata sheria za usalama barabarani

4 September 2025, 16:02

Sajent Khalid Mgaya kutoka ofisi ya Mkuu wa usalama barabarani Mkoani Kigoma akitoa elimu ya usalama barabarani, Picha na Hamis Ntelekwa

Ofisi ya usalama barabarani Mkoani Kigoma imesema itaendelea kutoa elimu na kuwachulia hatua za kisheria maredereva bodaboda wanaokiuka sheria za usalama barabarani

Na Orida Sayon

Vijana wanaofanya shughuli za usafirishaji maarufu bodaboda katika Manispaa ya Kigoma Ujiji  wameshauriwa  kufuata kanuni na sheria za usalama barabarani ikiwemo kuwa leseni ili waweze kufanya kazi zao bila usumbufu.

Hayo yameelezwa na Sajent Khalid Mgaya kutoka ofisi ya Mkuu wa usalama barabarani Mkoani Kigoma ambapo amesisitiza umuhimu wa madereva wa vyombo vya moto maarufu bodaboda kuwa na leseni ili kufanya kazi kwa uhuru na kuepusha matukio ya ajali barabarani.

Sauti ya Sajent Khalid Mgaya kutoka ofisi ya Mkuu wa usalama barabarani Mkoani Kigoma

Sajent  Khalid Mgaya amesema jeshi la polisi kitengo cha usalama wataendelea kutoa elimu, kuonya na kutoa adhabu kwa wasiozingatia kanuni za usalama.

Sauti ya Sajent Khalid Mgaya kutoka ofisi ya Mkuu wa usalama barabarani Mkoani Kigoma

Baadhi ya vijana ambao ni maafisa usafirishaji maarufu bodaboda wameeleza uelewa wao kuhusu umuhimu wa kuwa na leseni katika shughuli zao za usafirishaji.

Sauti ya baadhi ya vijana ambao ni maafisa usafirishaji maarufu bodaboda

Hayo yamejili katika Semina iliyoandaliwa na Shirika la Joy in The Harvest likiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kuelekea mashindano ya ligi ya DK. Livingstone Cup ikilenga kutoa elimu ya vitendo vya ukatili, maambukizi ya virusi vya ukimwi na kukuza vipawa kwa vijana Mkoani Kigoma kama anavyoeleza mkurugenzi wa shirika la Joy in the harvest Mwenge Muyombi