Joy FM

Wakristo watakiwa kuombea uchaguzi mkuu Kasulu

3 September 2025, 12:20

Baadhi ya waumini wa dini ya kikristo wa kanisa la Anglikana parish yakabanga Mjini Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Wakati uchaguzi Mkuu ukitarajia kufanyika Oktoba 29, 2025, waumini wa kikristo wametakiwa kuendelea kuliombea amani Taifa ili uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu

Na Hagai Ruyagila

Waumini wa Dini ya Kikristo Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma, wametakiwa kushiriki kikamilifu katika maombi kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu, ili taifa lipate viongozi bora wenye hofu ya Mungu, waadilifu na uzalendo watakaosimamia maendeleo ya nchi kwa haki na usawa.

Wito huo umetolewa na Askofu Mstaafu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Sadock Makaya wakati wa ibada ya sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika kanisa la anglikana Parishi ya Kabanga wilayani humo.

Katika hotuba yake, Askofu Makaya amewataka waumini hao kutumia kipindi hiki kuombea amani, mshikamano wa taifa na uchaguzi huru na wa haki huku akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wanaosimamia maslahi ya wananchi badala ya kufuata ushabiki wa kisiasa.

Sauti ya Askofu Mstaafu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Sadock Makaya
Mkurugenzi wa kanisa la Anglikana Kanda ya Kasulu Mjini, Canon James Bigombo, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kanisa la Anglikana Kanda ya Kasulu Mjini, Canon James Bigombo, ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la hilo Parish ya Murusi, ameeleza kuwa viongozi wa dini wana wajibu wa kuhakikisha waumini wao wanashiriki katika mchakato wa uchaguzi kwa njia ya amani, sala na uhamasishaji wa maadili mema.

Sauti ya Mkurugenzi wa kanisa la Anglikana Kanda ya Kasulu Mjini, Canon James Bigombo

Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo nao wameeleza umuhimu wa kuombea uchaguzi huo na madhara ya nayoweza kujitokeza endapo jamii kama haitaombea uchaguzi huo.

Sauti ya baadhi ya waumini waliohudhuria ibada

Uchaguzi mkuu wa oktoba 29 mwaka huu unatarajiwa kuvuta hisia za wengi, huku viongozi wa dini wakihimizwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha unafanyika kwa amani, haki na utulivu wa kitaifa.