Joy FM
Joy FM
3 September 2025, 08:49

Serikali Mkoani Kigoma imeanza kuchukua hatua kuhusu mgogoro wa eneo la hekta 10,000 ambalo wananchi wa kijiji cha Ruchugi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wanadaiwa kuvamia eneo la mwekezaji kampuni ya FAZENDA ambayo imekusudia kuwekeza katika mradi wa kilimo huku kutakiwa kuondoka ili mwekezaji aanze shughuli zake.
Na Orida Sayon
Zaidi ya wananchi 800 wanaoishi katika eneo la Ruchugi katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wameomba serikali kuwapatia eneo la kuishi na kufanya shughuli za kilimo ili kupisha shughuli za uwekezaji katika eneo hilo.
Hayo yamejili katika mkutano kati ya wananchi na Mkuu wa wa Mkoa wa Kigoma IGP mstaafu Simon Nyakoo Sirro uliofanyika leo katika eneo la Ruchugi Wilayani Uvinza uliolenga kutoa maelekezo kuhusu kupisha eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji.
Kwa mujibu wa mkutano uliofanyika mnamo mwezi August 2025 wananchi wanaofanya shughuli zao walipaswa kuhama eneo hilo ndani ya siku 14 .
Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinah Mathamani ambapo amesema eneo hilo ni miongoni mwa maeneo ya uwekezaji na Halmashauri imetekeleza sera ya serikali ya uwekezaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP mstaafu Simon Sirro ametamatisha mkutano huo kwa kutoa maelekezo kwa wananchi kuendelea na shughuli zao huku watendaji wakifanya mapitio na mwekezaji.
Eneo hilo la uwekezaji lipo katika makao makuu ya Wilaya ya Uvinza ikichukua jumla na hekari elfu 10 likitarajiwa kufanyika uwekezaji wa kilimo na kampuni ya FAZENDA Tanzania Limited.