Joy FM
Joy FM
14 August 2025, 13:22

Kampuni ya DongFang Electric (DEC) imefanikiwa kuchepusha maji ya mto Malagarasi katika eneo la Igamba kijiji cha Mwamila wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ili kuanza ujenzi wa tuta la bwawa la kuzalisha umeme kutoka Mto Malagarasi.
Na Orida Sayon
Mkurugenzi wa Shirika la umemem Tanzania (TANESCO) kanda ya magharibi Mhandisi Richard Swai amemuagiza msimamizi wa ujenzi wa mradi umeme kwenye chanzo cha mto maragalasi kumsimamia mkandarasi ili mradi ukamilike kwa wakati.
Hayo yamejili katika hafla fupi ya kufunga na kuchepusha mto malagarasi uliopo wilayani uvinza ili kupata sehemu kavu kwa ajili ya ujenzi wa tuta litakalo peleka maji katika mitambo ya chanzo cha kuzalish umeme.
Mhandisi Swai amesema kukamilika kwa mradi huo kutaweza kunufaisha mkoa wa kigoma na nchi nzima kwani utaongeza mega watt 49.5 kwenye grid ya taifa.

Naye Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi huo Han Wel ameeleza kuwa uchepushaji wa mto ni hatua ya kwanza katika utekelezaji wa mradi huo na hivyo matarajio yao ni kukamilisha kwa waakati na kunufaisha maeneo yaliyokaribu na mradi huo.
Baadhi ya wananchi kutoka vijiji vinavyozunguka mradi huo akiwemo Afisa mtendaji wa kata ya kazuramimba Bi.Naomi Andrew wanaeleza watakavyonufaika na mradi huo.
Ujenzi wa mradi wa chanzo cha kuzalisha umeme katika mto malagarasi ulianza kutekelezwa April 2024 na unatarajiwa kukamilika mwezi oktoba 2027.