Joy FM

Wanahabari wapewa mafunzo ya usalama wakati wa uchaguzi

13 August 2025, 15:57

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya usalama kwa waandishi wa habari, Picha na Emmanuel Senny

Kuelekea uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais, Waandishi wa habari Mkoani Kigoma wamepewa mafunzo ya usalama kazini hasa kipindi cha uchaguzi

N a Josephine Kiravu

Wanahabari Mkoani Kigoma wamepatiwa mafunzo ya namna ya kujilinda wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kipindi cha kampeni hadi uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Zaidi ya wanahabari 20 kutoka vyombo mbalimbali wamekusanyika ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kupata mafunzo yanayolenga usalama wa waandishi hasa kipindi cha uchaguzi na kueleza umuhimu wa mafunzo hayo.

Sauti ya wanahabari wa Kigoma
Wanahabari kuoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya usalama kwa waandishi wa habari, Picha na Emmanuel Senny

Katibu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma, Mwajabu Hoza amesema mafunzo hayo ni muhimu huku akiwataka wadau wengine kujitolea kufadhili mafunzo kwa wanahabari kwani kufanya hivyo itawaongezea ufanisi katika utendaji kazi wao.

Sauti ya Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kigoma Mwajabu Hoza

Mwenzeshaji wa mafunzo hayo ambae pia ni mwanahabari Adela Madyane anaeleza mapokeo ya wanahabari pamoja na changamoto wanazokumbana nazo.

Sauti ya Mwenzeshaji wa mafunzo hayo ambae pia ni mwanahabari Adela Madyane

Mafunzo hayo yanalenga kuwafikia wanahabari wengi zaidi huku matarajio ya kiwa ni kuongezeka kwa ufanisi kipindi hiki cha uchaguzi pamoja na kupunguza athari ambazo zimewahi kujitokeza kwa baadhi ya wanahabari.