Joy FM

DC Uvinza apiga simu TEMESA kivuko kutofanya kazi

13 August 2025, 09:59

Muonekano wa kivuko kikiwa katika mto Malagarasi, Picha na Mtandao

Mkuu wa Wilaya Uvinza Mkoani Kigoma Mh. Dinnah Mathaman ameagiza TEMESA kufanya ukarabati wa kivuko cha Ilagala ili kurejesha usafiri kwa wananchi ambao hutegemea usafiri huo kwenda katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Na Kadislaus Ezekiel

Wananchi wa Kata nane wa Jimbo la Kusini Mkoani Kigoma, wamekosa mawasiliano na shughuli za uzalishaji mali kusimama baada ya kivuko kilichokuwa kinatumika kuwavusha katika eneo la Mto MalagarasiKata ya Ilagala kuharibika wakati kikifanya kazi kwa zaidi ya siku tano na kusababisha adha kubwa ya kukosa usafiri na baadhi ya huduma za kijamii kusimama.

Hi si mala ya kwanza kivuko hiki kuharibika na kusababisha shughuli za uzalishaji kusimama hasa kilimo, usafirishaji na biashara kwa wananchi wa kata nane wanaotegemea kuvuka eneo hili.

Kutokana na kuharibika kivuko hiki kwa zaidi ya siku sita wananchi wameomba hatua za halaka zifanyike kuhakikisha kivuko kinakuwa sana na kuendelea na kazi.

Kutokana na uharibifu wa kivuko hiki, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinna Mathamani amefanya ziara ya kushtukiza na kuzungumza na wananchi kuwatia moyo.

Kisha akatoa maelekoezo ya Serikali kwa wakala wa ufundi na umeme Tanzania (TEMESA) ambao ndio wasimamizi.

Sauti ya Kadislaus Ezekiel