Joy FM

Wasimamizi wa uchaguzi zitangatieni sheria za INEC

7 August 2025, 16:13

Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya uchaguzi Halmashauri ya Mji Kasuluwakipatiwa mafunzo, Picha na Hagai Ruyagala

Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kasulu Mji Nurfus Aziz ametoa maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata kuhakikisha wanafuata miongozi ya Tume ya uchaguzi

Na Hagai Ruyagila

Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kutoa mafunzo sahihi kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru, haki na uwazi.

Wito huo umetolewa na Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kasulu Mji Nurfus Aziz wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata yaliyofanyika Mjini Kasulu.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo Bw. Aziz amesisitiza umuhimu wa utoaji mafunzo sahihi kwa Wasimamizi wa vituo, Wasimamizi wasaidizi wa vituo na Makarani waongozaji wawapiga kura ili kufanikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa kuaminika.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kasulu Mjini Nurfus Aziz, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema wasimamizi hao ni kiungo muhimu kati ya Tume na wananchi, hivyo ni lazima wajenge imani kwa jamii kwa kutekeleza wajibu wao kwa uwazi na haki.

Sauti ya Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kasulu Mji Nurfus Aziz

Afisa uchaguzi Halmashauri ya Mji Kasulu Daniel Kaloza amesema kazi yao ya utoaji mafunzo imekamilika na anaimani na watendaji hao wa tume kufanya kazi nzuri ili kufanikisha uchaguzi unafanyika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Sauti ya Afisa uchaguzi Halmashauri ya Mji Kasulu Daniel Kaloza

Mwakilishi wa Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata katika Halmashauri hayo Twallybu Yasini amesema watafanya kazi hiyo kwa ulewedi na kufuata sheria na miongozo ya tume huru ya taifa ya uchaguzi.

Sauti ya Mwakilishi wa Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata katika Halmashauri hayo Twallybu Yasini

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu ambapo Tume huru ya taifa ya uchaguzi imeendelea kusisitiza umuhimu wa mafunzo kwa watendaji wake ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, amani na kuzingatia misingi ya demokrasia.