Joy FM
Joy FM
7 August 2025, 11:26

Siku chache baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza katika uchaguzi wa kura za maoni, Mgombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjiji Kirumbe Ng’enda ametoka hadharani na kuwashukuru wajumbe na kuweka wazi kilichompa ushindi huo
Na Tryphone Odace
Mgombe ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM, Jimbo la Kigoma Kirumbe Shaban Ng’enda amesema miongoni mwa vitu vilivyompa nguvu ya kuendelea kuaminika ndani ya chama hicho ni pamoja na usimamizi wake katika kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inatekelezwa ndani ya jimbo hilo.
Ngenda amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma na kueleza kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo umesaidia wananchi kupata huduma karibu ikiwemo maji na vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha amesema kuwa Mjiji wa Kigoma ulikuwa na makorongo ambayo yalikuwa kikwazo kwa wananchi na hivyo kutokana na juhudi na ushuikiano wake na viongozi wengine wameweza kufanikisha kuyaziba na kuhakikisha usalama wa wananchi unaendelea bila kikwazo kwenye maeneo yao.
Hata hivyo amewashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumpigia kura nyzilizowezesha yeye kuibuka mshindi katika kura za maoni.