Joy FM
Joy FM
5 August 2025, 17:17

Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye amemteua Nestor Ntahontuye kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo
Na Bukuru Elias Daniel
Waziri wa zamani wa fedha na hazina wa Burundi Nestor Ntahontuye ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa Burundi katika mabadiliko mapya ya serikali ya Rais Evariste Ndayishimiye.
Nestor Ntahontuye anachukua nafasi ya Jenerali Gervais Ndirakibuca ambaye amechaguliwa kuwa spika wa bunge la Seneti nchini Burundi.
Akiwa na umri wa miaka 47, Nestor Ntahontuye ana shahada ya uzamili katika takwimu.Alizaliwa katika jimbo la zamani la Ruyigi mwaka 1978, sasa Buhumuza
Kuanzia tarehe 09/12/2024, aliteuliwa kuwa waziri wa fedha na hazina ya nchi akishikilia nyadhifa hizilo kwa muda wa miezi minane
Katika uchaguzi wa 2020, alichaguliwa kuwa mbunge anayewakilisha Ruyigi. Katika nafasi hiyo ya miaka minne, aliongoza kamati ya kudumu ya bunge ya uchumi