Joy FM
Joy FM
5 August 2025, 13:21

Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na watoto wakishirikiana na idara ya maendeleo ya jamii Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wamewataka wananchi kuacha matukio ya ukatili hasa ubakaji na ulawiti kwa watoto na wanawake na kuhakikisha wanaripoti matukio ya ukatili kwa wakati ili kuhakikisha watuhumiwa wanachukuliwa hatua za kisheria mara moja.
Katika mkutano wa kuelimisha jamii juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia katika mji mdogo wa Ilagala Wilayani Uvinza, Mkaguzi Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilayani humo Winifrida Joram amekemea baadhi ya wazazi kuwaingilia watoto kimwili kwa imani za kishirikina wakiamini kupata mali.
Ofisi ya Idara ya Maendeleo ya jamii Wilayani Uvinza, imesisitiza wazazi kuwa na malezi bora kwa watoto, na kuhakikisha wanajikita katika kujenga uchumi ili kumdu mahitaji ya familia.
Ukamilifu wa malezi kwa watoto, husaidia kupunguza matukio ya ukatili kwa na kujenga kizazi chenye hofu ya Mungu na imara.