Joy FM
Joy FM
24 July 2025, 15:30

Halamshauri ya Wilaya Kasulu imepanga kuzalisha miche milioni moja ya kahawa ili kutoa fursa kwa wakulima wengi kufikiwa na kuongeza tija ya uzalishaji wa zao hilo.
Na Emmanuel Kamangu
Wakulima wa zao la kahawa katika kijiji cha Kibirizi kata ya Buhoro Halamshauri ya Wilaya ya Kasulu wameishukuru Serikali kwa kuwapatia miche pamoja mbegu bora za kisasa za kahawa aina ya Arabica mbegu zinayotajwa kuwa bora tofauti na mbegu za zamani.
Baadhi ya wakulima hao akiwemo Bi. Lidia Kasimiri wakizungumza na Redio Joy mara baada ya kutembelewa na Kaimu Mkuu idara ya Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya kuona maendeleo ya zao la kahawa katika kata ya Buhoro wameishukuru Serikali kwa kuwapatia bure miche ya kisasa.

Naye Mwalimu wa Taaluma Shule ya Msingi Buhoro Bw. Stanslaus Petro amesema kilimo cha zao la kahawa katika shule hiyo kimewasaidia sana kuongeza kipato cha shule na kupelekea wanafunzi kupata uji shuleni hapo.
Kaimu Mkuu idara ya Kilimo katka halmashauri hiyo Bw. Masumbuko Kelemwa akiwa katika ziara hiyo ya kutembelea mashamba ya wakulima ya kahawa kata Buhoro amesema ugawaji bure wa miche ya kahawa aina ya Arabica umeleta matokeo chanya kwa kuongeza idadi ya wakulima kutoka 50 hadi kufikia 350 ndani ya mwaka mmoja na hii ikichangiwa na wakulima wengi kuvutiwa na mbegu hiyo ambayo hustahimili magonjwa na kuzaa kwa wingi.
