Joy FM

Wajasiriamali watakiwa kuzalisha bidhaa bora

23 July 2025, 12:30

Muonekano wa bidhaa za bidhaa za wajasiriamali, Picha na Mtandao

Serikali imewataka wajasiriamali kuendelea kuboresha bidhaa zenye ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.

Na Michael Mpunije

Vikundi vya wajasiriamali katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma, vimetakiwa kuongeza uzalishaji ili kupata masoko ya nje ya nchi.

Akizungumza na wa wajasiriamali wa kikundi cha Masega kinachojihusisha na ufugaji nyuki pamoja na kikundi cha ufugaji kuku katika kata ya Nyumbigwa, Katibu Tawala Wilaya ya Kasulu Bi, Theresia Mtewele ametoa wito wa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuzalisha kwa wingi bidhaa zenye Ubora.

Amesema maafisa maendeleo ya jamii wanatakiwa kushirikiana na watendaji wa kata kuhakikisha wanafuatilia na kutoa elimu katika vikundi vya wajasiriamali ili viweze kuzalisha kwa tija kwa ajili ya manufaa yao.

Sauti ya Katibu tawala Wilaya ya Kasulu Bi, Theresia mtewele

Mkuu wa idara ya kilimo mifugo na uvuvi, Halmashauri ya mji kasulu Sabinus chaula amesema wataendelea kushirikiana katika kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinapata soko la uhakika ili kufikia malengo ya vikundi.

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Halmashauri ya Mji Kasulu Sabinus Chaula

Baadhi ya wajasiriamali katika kikundi cha masenga kinachojihusisha na ufugaji nyuki pamoja na kikundi cha ufugaji wa kuku wamesema wanayo matarajio makubwa ya kulea famili zao kupitia katika miradi wanayo itekeleza.

Sauti ya Baadhi ya wajasiriamali katika kikundi cha Masenga