Joy FM

Mashine nane za uvuvi zaporwa Ziwa Tanganyika

21 July 2025, 15:59

Muonekano wa mwalo wa Katonga Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Mtandao

Wavuvi wanaofanya shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Tanganyika wameomba Seriakali kushughulikia vitendo wizi na uhalifu ndani ya ziwa hilo

Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kuwavamia na kupora mashine nane za uvuvi katika mwalo wa Katonga Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma ambapo baadhi ya wavuvi wamelitupia lawama Jeshi la Polisi kutokana na vitendo hivyo kujirudia mara kwa mara bila kudhibitiwa.