Joy FM
Joy FM
14 July 2025, 13:03

Serikali ya Mkoa wa Kigoma imesema itahakikisha hakuna mtu atakayevunja amani na kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unakuwa salama.
Na Josephine Kiravu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewatahadharisha wenye nia ya kuvuruga amani na kuwataka kuacha mara moja kwani Serikali ipo macho na haitovumilia uvunjifu wowote wa amani.
Taarifa zaidi na Josephine Kiravu
Mkuu wa mkoa amesema hayo katika mwendelezo wa ziara yake ambapo amesisitiza kuchukua hatua kali dhidi ya wahalifu huku akiitaka jamii pia kutoa taarifa pale wanapobaini uwepo wa watu hao.
Na hapa akasisitiza kuhusu suala la uwekezaji akiwataka viongozi wa halmashauri ya Kakonko kutenga maeneo huku akitoa wito pia kwa wale wenye nia ya kuwekeza kujitokeza na kufanya uwekezaji.
Katika ziara yake kwenye halmashauri za Mkoa wa Kigoma Mkuu wa Mkoa amekuwa akihimiza suala la uwekezaji pamoja na kuongeza kasi kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kutilia mkazo kuhusu kulinda amani ya nchi.