Joy FM
Joy FM
14 July 2025, 12:39

Wajibu wa wananchi katika kudhibiti rushwa ni muhimu sana ili kuhakikisha kuwepo kwa utawala bora, uwazi, na maendeleo ya kweli katika jamii.
Na Timotheo Leonard
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kigoma imesema miongoni mwa majukumu yake ni kuhakikisha wananchi wanatambua wajibu wao wakusimamia miradi ya serikali inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Ibrahim Sadiki Mkuu wa Dawati la Elimu kwa umma TAKUKURU Mkoa wa Kigoma wakati akizungumza na redio Joy Fm kupitia kipindi cha Goodmorning Kigoma, na kuwa hivi sasa wanatoa elimu kwa wananchi juu ya kutambua umuhimu wa kusimamia miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Ghanima Thabiti ambaye ni Afisa wa Dawati la Elimu kwa Umma TAKUKURU Mkoa wa Kigoma amesema wananchi hawanabudi kushirikiana kutoa taarifa za vitendo vya rushwa.
Aidha, Katika mapambano dhidi ya rushwa Tanzania imeendelea kupiga hatua kutoka nafasi ya 87 kati ya nchi 180 kwa mwaka 2023 hadi nafasi ya 82 kwa mwaka 2024 kwa nchi zilizofanyiwa utafiti baada ya kupata alama 41