Joy FM
Joy FM
8 July 2025, 17:26

Mkoa wa Kigoma unaendelea kufanya vizuri kitaifa katika uzalishaji wa zao la Muhogo ambapo makadirio kwa mwaka hufikia hadi tani milioni 1.2 za muhogo mkavu na mbichi huku matarajio ikiwa ni kufikia zaidi ya tani milioni 3 ifikapo mwaka 2030.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amezitaka Halmashauri za Wilaya Kasulu kutenga eneo kubwa la uwekezaji wa zao la kilimo cha muhogo ili kuleta mapinduzi makubwa ya uzalishaji kutokana na utayari wa wawekezaji kutoka china ambako kwa sasa soko la zao hilo ni kubwa.