Joy FM

Mila, desturi kikwazo kwa wanawake kuwania uongozi

3 July 2025, 10:57

Baadhi ya viongozi wanawake kutoka vyamba mbalimbali na wazee kimila, Picha na Hamis Ntelewa
Makala inayoangazia mila na desturi zilivyo kikwazo kwa wanawake kushiriki kuwania nafasi za uongozi

Katika jamii nyingi, mila na desturi zimekuwa nguzo muhimu zinazotambulisha utamaduni na urithi jamii husika. Hata hivyo, mila hizo zimekuwa pia kikwazo kikubwa kwa wanawake wengi, hasa linapokuja suala la uongozi ambapo zimekuwa zikiwanyima wanawake nafasi ya kushiriki kikamilifu katika uongozi wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na hata kiimani.