Joy FM
Joy FM
26 May 2025, 16:32

Viongozi wa dini Nchini wamehimizwa kuendelea kuliombea Taifa hasa kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu.
Na Josephinr Kiravu
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa dini Kutumia majukwaa yao kuhimiza amani ikiwa ni pamoja na kusisitiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kujenga taifa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu katika harambee ya kuendeleza ujenzi wa kanisa la FPCT Majengo lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.
Katika ibada hiyo, Kaimu Askofu mkuu FPCT Elias Simon anawakumbusha waumini kumtanguliza Mungu katika Kila jambo.
Pamoja na mafundisho hayo jambo kubwa ambalo limewakutanisha ni harambee ya kuendeleza ujenzi wa kanisa hilo ambalo linahitaji zaidi ya shilingi milioni mia saba hadi kukamilika kwake.

Katika harambee hiyo salamu za Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zinawasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye msisitizo ukiwa kwa viongozi wa dini kutumia majukwaa yao kuhimiza amani.
Harambee hiyo imeenda sambamba na maombi ya kuliombea taifa huku Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amechangia milioni thelathini.