Joy FM
Joy FM
26 May 2025, 16:18

Wakati Taifa likeelekea katika uchaguzi Mkuu, wakristo wameaswa kuendelea kuombea amani
Na Hagai Ruyagila
Waumini wa Dini ya Kikristo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuliombea taifa kuelekea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ocktoba mwaka huu ili ufanyike kwa amani na utulivu.
Akizungumza kwenye ibada takatifu ya ufunguzi wa kanisa la Anglikan Dinal ya Mwilamvya, Askofu wa Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta amesema waumini pamoja na viongozi wa dini wanapaswa kutumia majukwaa yao kuliombea taifa ili uchaguzi Mkuu mwaka huu ufanyike kwa amani.
Aidha Askofu Bwatta amepiga marufuku viongozi wa vyama vya siasa kufanya kampeni za uchguzi katika nyumba za ibada.
Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imejipanga kuhakikisha inaimarisha ulinzi na usalama huku akitoa wito kwa waumini kuendelea kuomba amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

Baadhi ya Waumini wa kanisa la Anglikana Mwilamvya wamesema niwajibu wao kuliombea amani taifa ili jamii iweze kuishi kwa upendo umoja na mshikamano.
