Joy FM

Baraza la madiwani lampongeza Rais Samia kwa uongozi wake

15 May 2025, 15:52

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wakiwa katika kikao Cha robo ya tatu ya Mwaka wa fedha 2024/2025, Picha na Hagai Ruyagila

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amepewa pongezi na kuchangiwa fedha kwa ajili kuchukua fomu ya kugombea Urais baada ya kazi yake iliyotukuka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Na Hagai Ruyagila

Baraza la Madiwani na Menejimenti ya halmashauri ya Wilaya ya Kasulu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake uliowezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mh. Elia Kagoma ameeleza namna baraza la madiwani katika halmashauri hiyo linavyotambua mchango wa Rais Dkt Samia suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mh. Eliya Kagoma akikabidhi mchango wa Shilingi milioni Moja kwa katibu wa CCM wilaya ya Kasulu Bi. Jenifer Shinguile, Picha na Hagai Ryagila.

Pongezi hizo zimeambatana na utoaji wa mchango wa shilingi milioni moja ili kumwezesha kuchukua fomu ya kugombea urais sanjari na kuunga mkono jitihada za Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini Mh. Vuma Hole.

Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mh. Elia Kagoma

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu Bi, Jenifer Chinguile kwa niaba ya chama amekiri kupokea mchango huo na kuahidi kufikisha kwenye uongozi kabla ya Kufanyika kwa Mkutano mkuu wa chama hicho.

Sauti ya Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu Bi, Jenifer Chinguile

Baraza la madiwani halmashauri wilaya ya Kasulu linajumla ya madiwani 9 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani na swali ambalo huenda kila mtu anajiuliza ni namna gani madiwani hao wameshiriki katika zoezi la kumpongeza Rais Samia pamoja na kutoa mchango wa kuunga mkono kuchukua fomu ya kugombea urais.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mh. Eliya Kagoma akikabidhi katibu wa mbunge mchango wa kuchukua fomu ili mpelekee Mbunge Mh . Vuma Hole, Picha na Hagai Ruyagila.

Jonas Abel Kaja ni diwani kata ya Rungwe mpya kupitia Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani alikuwa na haya ya kusema.

Sauti ya Jonas Abel Kaja ni diwani kata ya Rungwe mpya kupitia Chama cha ACT Wazalendo