Joy FM
Joy FM
24 April 2025, 12:33

Tume huru ya Taifa imeendelea kusimamia ugawanyaji wa majimbo yalikuwa yanaonekana makubwa na hivyo kugawanywa ili kuweza kusogeza huduma kwa wananchi
Na Lucaa Hoha
Wadau wa uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wamepitisha muhtasari kutoka tume huru ya Taifa ya uchaguzi kuhusu mapendekezo yaliyowasilishwa na wananchi ya kuligawa jimbo la kasulu Vijijini lengo likiwa ni kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi.
Nathanael Ndelema ni Diwani wa Kata ya Nyamyusi akizungumza kwa niaba wa wadau hao wa uchaguzi kwenye kikao kilichowakutanisha viongozi mbalimbali akiwemo mwakilishi wa mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina.
Awali mkurugenzi wa huduma za sheria ya tume huru ya Taifa ya uchaguzi Mtibora selemani ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa tume huru ya Taifa ya uchaguzi ametaja majina mapya ya jimbo na kata zitakazounda jimbo hilo pindi watakapoligawa jimbo la Kasulu vijijini
Hamza Selemani ni Mwakilishi wa mjumbe wa tume huru ya Taifa ya uchaguzi amesema kwa mjibu wa ibara ya 75 kifungu kidogo cha 4 na 74 kifungu kidogo cha 6C za katiba ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 10 kifungu kidogo cha 1D cha sheria ya tume huru ya taifa ya uchaguzi 1 ya mwaka 2024 tume ina jukumu la kuchunguza na kuigawa jamhuri ya muungano katika majimbo ya uchaguzi.