Joy FM

Wajasiriamali, wafanyabiashara watakiwa kuwa wabunifu Kigoma

28 March 2025, 16:38

Baadhi ya wajasiriamali waliopatiwa mafunzo, Picha na Michael Mpunije

Serikali itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na mashirika mbalimbali kwa kutoa ujuzi wa namna bora ya kukuza biashara zao.

Na Michael Mpunije

Wajasiriamali na wafanyabiashara mkoani Kigoma wametakiwa kuwa wabunifu ili kuingia katika soko la biashara lenye kuleta tija na mafanikio katika biashara zao kwa kutambua sheria za kazi  ili kukuza na kuinua uchumi wao..

Hayo yamejiri wakati wa kuhitimisha mafunzo ya wiki mbili ya kuwajengea uwezo viongozi wa taasisi na vikundi mbalimbali vya wafanyabiashara  mafunzo ambayo yamefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani ILO kupitia mradi wa Kigoma Pamoja kwa kushirikiana na shirika la Enabel wanaotekeleza mradi  Wezesha Binti kwa lengo ya kuwajengea uwezo vijana na wanawake kutambua mbinu bora za kuanzisha biashara na namna ya kukuza biashara zao.

Mratibu wa miradi wa pamoja tuwalee katika mkoa wa kigoma kutoka shirika la Kazi duniani Nureen Toloka amesema ameeleza dhima kuu ya mafunzo hayo.

Sauti ya Mratibu wa miradi wa pamoja tuwalee katika mkoa wa kigoma kutoka shirika la Kazi duniani Nureen Toloka

Akifunga mafunzo hayo, Kaimu katibu tawala Mkoa wa Kigoma Bw.Deogratius sangu amesema serikali itaendela kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na mashirika mbalimbali kwa kutoa ujuzi wa namna bora ya kukuza biashara zao ziwe zenye kuleta tija kwa maendeleo ya taifa na mtu binafsi.

Sauti ya Kaimu katibu tawala Mkoa wa Kigoma Bw. Deogratius sangu

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo wameeleza namna mafunzo hayo yatakavyowasaidia katika biashara zao na kuwa watakuwa waalimu wazuri katika kutoa elimu kwa watu wengine.

Sauti ya Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo wameeleza namna mafunzo hayo yatakavyowasaidia
Pichani ni Kaimu katibu tawala Mkoa wa Kigoma Bw.Deogratius sangu nabaadhi ya washiriki wa mafunzo, Picha na Michael Mpunije