

27 March 2025, 08:34
Na Kadislaus Ezekeiel
Kamati Ya Ulinzi na Usalama Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, Imekanusha Uwepo wa Mapigano ya kutumia Silaha za jadi Kati ya Wananchi na Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale, Wakipinga Vitongoji vya MAHASA na KABUKUYUNGU Katika Kijiji Cha KALELANI Kata ya Buhingu, Wakipinga Kupisha Eneo Hilo ili kupisha shughuli za uhifadhi wa Wanyama Ikiwemo SOKWE MTU, Wanaohifadhiwa katika hifadhi hiyo.
Ni mwezi Mmoja umepita wananchi zaidi ya kaya 300, Za Vitongoji vya MAHASA na KABUKUYUNGU, Katika Kijiji cha KALELANI Wilayani Uvinza kutakiwa kuondoka maeneo hayo, kupisha shughuli za uhifadhi wa wanyama poli ikiwemo sokwe mtu, ikiwa ni baada ya Serikali kulipa fidia kaya zaidi ya 200, Kiasi cha Shilingi Bilioni 1.68, Huku kaya zaidi ya 170 zikigomea uthamini na kugoma kupisha eneo hilo.
Wakiwa Katika Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama, na Wadau wa Uhifadhi wa Mazingira Katika Wilaya ya Uvinza, Wakiongozwa na Kaimu mkuu wa Mkoa wa Kigoma, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinna Mathamani, amesema taarifa ambazo zimesambaa za uwepo wa mapigano kwa wananchi waliogoma kuondoka eneo hilo, Hazina ukweli na wananchi wapo salama wakiendelea na shughuli za uzalishaji mali.
Kuhusu Kaya 170 ambazo ziligoma kupisha eneo hilo ili shughuli za uhifadhi ziendelee, Mkuu wa Wilaya Dinna Mathamani, amesema linafanyiwa kazi Kupata maamuzi kufuatia vikao vinavyoendelea.
Hatahivyo uongozi wa hifadhi ya milima ya Taifa Mahale, Chini ya Kaimu mkuu wa hifadhi Afisa mhifadhi mkuuHaridi Mgofi, amesema hadi sasa asilimia 90 ya waliolipwa fidia tayari wamepisha eneo hilo na kuondoa mwingiliano kati ya binadamu na wanyama.