

26 March 2025, 16:35
Kikundi cha Upendo kilichopo chini ya Kanisa la Pentekoste Motomoto PMC Kibirizi kimetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wazee wanaoishi kambi ya Silabu Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma
Na Orida Sayon
Imekuwa ni utaratibu na desturi kwa kikundi cha upendo chiniya mchungaji Emmanueli Michael Kambi wa kanisa laPentekoste motomoto PMC lilopo Kibiriz katika manispaa ya Kigoma Ujiji kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji kama walemavu, wajane na yatima pamoja na wazee.
Kikundi hiki kimefika katika makao ya wazee wasiojiweza cha Silabu na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mavazi naviatu kwa wazee hao nahapakatibumsaidizi wakikundi hicho John Mahumbenge amesema lengo la uwepo wa kikundi hichona kutoa wito kwa wadau kuendelea kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Saauti ya Katibu wa kikundi ch upendo John Kahumbege
Baadhi ya wazee kutoka kambi ya Silabu wameeleza hisia zaoza shukurani kwa kikundi hicho na kwa wadau wengine
Saaauti za baadhi ya wazee
Nyanguba Majinge ni afisa ustawi wa jamii Msaidizi kwenyemakao hayo amesema jukumu la kuwatunza wazee ni la kilamwanajamii na kueleza baadhi ya changamoto zinazowakabilikatika kuhakikisha ulinzi kwa wazee hao.
Sauti ya Afisa ustawi msaidizi
Jumla ya wazee 25 wanalelewa na kutunzwa katika makaao yawazee wasiojiweza Silabu wanaume wakiwa 14 na wanawake11na kipo chini ya wizara ya maendeleo ya jamii idara ya ustawi wa jamii.