Joy FM

DC, wananchi sauti moja mapambano dhidi ya m-pox

25 March 2025, 09:35

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kausulu (kulia) wakiwa katika kikao kikao cha kamati ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu.Picha na Michael Mpunije

Baadhi ya wananchi wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba idara ya afya wilayani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kujikinga na ugonjwa wa MPOX.

Na Michael Mpunije.

Wananchi hao wamesema Elimu kuhusu tahadhari za ugonjwa wa Mpox bado haijawafikia wananchi wengi hivyo ni muhimu wataalamu wa afya kutoa elimu katika maeneo ya mikusanyiko.

Wamesema ili kuhakikisha jamii inakuwa salama ni muhimu wananchi kuwa na desturi ya kusoma matangazo mbalimbali ili kuendelea kuchukua tahadhali kuhusu ugonjwa huo.

wananchi

Kwa upande wake mratibu wa Elimu ya afya kwa Umma halmashauri ya wilaya ya Kasulu,Amani Mkemwa amesema wanaendelea kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kupitia kwa Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kuhamasisha jamii kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono,kukumbatiana pamoja na kuzingatia kanuni zote zinazotolewa na wataalumu wa afya.

Mratibu wa Elimu ya afya kwa Umma halmashauri ya wilaya ya Kasulu,Amani Mkemwa

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akizungumza kwenye kikao cha kamati ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu  amesema wamekuwepo washukiwa kadhaa wa ugonjwa wa MPOX katika wilaya hiyo ambapo amesisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu