Joy FM

Madereva wapigwa msasa wilayani Kasulu

20 March 2025, 19:59

Baadhi ya Madereva wa Pikipiki na wakufunzi kutoka Chuo Cha taifa Cha usafirishaji NIT kupitia kituo Cha kikanda Cha umahiri katika usalama barabarani pamoja na jeshi la polisi kikosi Cha usalama barabarani wilaya ya Kasulu.Picha na Hagai Ruyagila

Madereva wa vyombo vya moto katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuwa madereva bora kwa kuchukua tahadhari wawapo barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Na, Hagai Ruyagila

Akitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki maarufu bodaboda na madereva wa bajaji Mjini Kasulu, Mkuu wa kituo cha kikanda cha umahiri katika usalama barabarani (NIT) kanda ya Afrika mashariki na kusini mwa Afrika Godlisten Msumanje, Amesema dereva bora anatakiwa kuwa makini wakati wote awapo barabarani ili kuepuka ajari zisizotarajiwa.

Godlisten Msumanje

Kwa upande wake kaimu mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Kasulu Willy Lupa amesema elimu ya usalama barabarani ni yamuhimu sana katika kupunguza ongezeko la ajari barabarani.

kaimu mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Kasulu Willy Lupa

Nao baadhi ya medeva wa pikipiki maarufu bodaboda na madereva wa bajaji wamesema kupitia mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza umakini barabarani katika  kuhakikisha wanaepukana na ajari zisizokuwa na ulazima.

Madereva

Mafunzo hayo yametolewa na Chuo Cha taifa cha usafirishaji NIT kupitia kituo chake cha kikanda cha umahiri katika usalama barabarani ambapo kimeandaa mafunzo hayo ya usalama barabarani kwa baadhi madereva wa pikipiki maarufu bodaboda na madereva bajanji katika halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma ili kuwasiaidi kufuata sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.