Joy FM

Kamati ya ushauri Kigoma RCC yaridhia mapendekezo ya ugawaji majimbo

18 March 2025, 15:56

Wajumbe wakishiriki katika baraza la ushauri la mkoa wa Kigoma RCC,-Picha na Josephine Kiravu

Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Kigoma imepitia na kuridhia kupeleka mapendekezo ya vikao vya DCC kuhusu ugawaji wa majimbo pamoja na kubadili majina ya baadhi ya majimbo kwa tume huru ya Taifa ya uchaguzi kulingana na muongozo waliotoa hivi karibuni.

Na Josephine Kiravu

Miongoni mwa majimbo yanayopendekezwa ni pamoja na Kigoma mjini kuwa majimbo mawili,  kasulu vijijini kupata majimbo mawili na Muhambwe pia kupata majimbo mawili.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amesema wamepitia kwa pamoja na kuridhia mapendekezo yote yapelekwe Tume huru ya Taifa ya uchaguzi kulingana na mwongozo uliotolewa na tume hiyo hivi karibuni.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye

Na hapa Afisa uchaguzi Mkoani Kigoma Husein Moshi amesema mapendekezo yamepokelewa ya kugawa majimbo pamoja na kubadili majina ya baadhi ya majimbo.

Sauti ya Afisa uchaguzi mkoani Kigoma

Kwa upande wake, Mstahiki meya Manispaa ya Kigoma ujiji akichangia hoja kwenye kikao hicho pamoja na Diwani wa kata ya Rubuga Omary Gindi wamesema ili kuleta changamoto ya kiuchumi ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji ni lazima kugawa jimbo la kigoma kuwa majimbo mawili.

Saauti ya Meya pamoja na Diwani wa Manispaa ya Kigoma ujiji

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na tume huru ya uchaguzi feb 26 mwaka huu vigezo vitakavyotumika kugawanya majimbo ni wastani wa idadi ya watu majimbo ya mjini kuanzia wastani wa watu laki 6 na halmashauri ni laki 4 huku hali ya uchumi ikitajwa pia ukubwa wa eneo husika sambamba na mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yaliyopo