Joy FM

NIT yatoa mafunzo ya usalama barabarani Kigoma

18 March 2025, 14:34

Mkuu wa kituo cha kikanda cha umahiri katika usalama barabarani- NIT kanda ya Afrika mashariki na kusini mwa Afrika Godlisten Msumanje katika mafunzo ya usalama barabarani kwa baadhi ya shule za msingi zilizopo Kasulu,-Picha na Hagai Ruyagila

Chuo cha Taifa cha usafirishaji NIT chatoa elimu ya usalama barabarani kwa wananchi mkoani Kigoma

Na Hagai Ruyagila

Chuo Cha taifa cha usafirishaji NIT kupitia kituo chake cha kikanda cha umahiri katika usalama barabarani kimeandaa mafunzo ya usalama barabarani kwa baadhi ya shule za Msingi halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma ili kuwasiaidi wanafunzi kufuata sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Katika kuendelea kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi ambazo zipo kando ya barabara Mkuu wa kituo cha kikanda cha umahiri katika usalama barabarani (NIT) kanda ya Afrika mashariki na kusini mwa Afrika Godlisten Msumanje amesema lengo la mafunzo hayo ni kupunguza ajali kwa watembea kwa miguu pamoja na watumiaji wa vyombo vya moto.

Sauti ya mkuu wa kituo cha kikanda cha umahiri kanda ya Afrika mashariki na kusini mwa Afrika Godlisten Msumanje

Aidha Msumanje amesema ni muhimu madereva kuepuka kutumia vilevi wanapokuwa katika safari zao ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Sauti ya Godlisten Msumanje

Copro Emmanuel Fussy kutoka jeshi la polisi kitengo cha dawati la elimu ya usalama barabarani wilaya ya Kasulu amesema wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za kuhakikisha wanapunguza ajali kwa watoto na wanafunzi wanapohitaji kuvuka barabara.

Sauti ya Copro Emmanuel fussy kutoka jeshi la polisi kitengo cha dawati la elimu ya usalama barabarani wilaya ya Kasulu

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya mbalimbali za msingi halmashauri ya mji kasulu wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kutambua umuhimu wa matumizi ya alama za barabarani.

Sauti za baadhi ya wanafunzi waliopata mafunzo

Katika halmashauri ya mji Kasulu Shule za msingi Kalema, Umoja, Murubona, Kiganamo na Kimobwa ni miongoni mwa shule ambazo zimenufaika na mafunzo hayo kwa siku ya kwanza.

Wanafunzi wakishiriki mafunzo ya usalama barabarani,-Picha na Hagai Ruyagila