Joy FM

Utekelezaji hafifu wa njia za kuimarisha usalama changamoto kwa wanafunzi shuleni

17 March 2025, 15:27

Kamishna wa elimu Tanzania Dkt Lyabwene Mtahabwa akito hotuba kwa niaba ya katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia katika uzinduzi wa programu ya utafiti tendaji kuhusu usalama na jumuishi katika elimu,-picha na Hagai Ruyagila

Serikali yabaini Utekelezaji hafifu wa njia za kuimarisha usalama wa wanafunzi kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi shuleni hasa wenye mahitaji maalumu

Na Hagai Ruyagila

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu sayansi na Taknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tamisemi, pamoja na Programu ya shule bora imebainisha changamoto mbali mbali zinazowakabili wanafunzi ikiwemo Utekelezaji hafifu wa kuimarisha usalama wa wanafunzi na msaada duni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Akizungumza katika uzinduzi wa programu ya utafiti tendaji kuhusu usalama na jumuishi katika elimu, Kamishna wa elimu nchini Tanzania Dkt Lyabwene Mtahambwa ametoa hotuba kwa niaba ya Katibu mkuu wizara wa elimu sayansi na teknolojia katika hafla hiyo iliyofanyika Mjini Kasulu Mkoani Kigoma

Dkt Lyabwene amesema usalama wa wanafunzi umekumbwa na changamoto huku wanafunzi wenye mahitaji maalum wakikosa haki zao kama watoto wengine.

Sauti ya Kamishna wa elimu Tanzania Dkt Lyabwene Mtahabwa

Kwa upande wake, Mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa wa Kigoma Bi. Paulina Ndigeza amesema utafiti huo umepokelewa kwa mikono miwili na wataendelea kuufanyia kazi ili kuboresha hali ya elimu katika maeneo yaliyokusudiwa.

Sauti ya Paulina Ndigeza

Naye Mwakilishi wa mkurugenzi wa elimu, Ofisi ya rais Tamisemi John Chekwaze amesisitiza kuwa utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha mbinu za utoji wa elimu nchi, ili kuhakikisha haki ya elimu inapatikana kwa kila mwanafunzi.

Sauti ya John Chekwaze

Awali Mratibu wa programu ya shule bora kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia Morice Mkhotya ameeleza lengo la utafiti huu ni kubaini changamoto zinazowakabili wanafunzi wote wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kupata suluhu bora na endelevu kwa changamoto hizo.

Sauti ya Mratibu wa programu ya shule bora Morice Mkhotya  

Kigoma ni miongoni mwa mikoa minne iliyochaguliwa kufanya utafiti wa mpango wa programu ya utafiti tendaji kuhusu usalama jumuishi katika elimu ambao umezinduliwa rasmi chini ya taasisi ya shule bora nchini ikiwa na lengo la kuwasaidia watoto wote nchini iwe wenye ulemavu au wasio na ulemavu ili kuhakikisha wanapata elimu bora pasi na changamoto yoyote