

4 February 2025, 10:13
Zikiwa zimetamatika siku 10 za kampeni ya msaada wa kisheria kwa mkoa wa Kigoma, wananchi wameiomba mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wanaotekeleza vitendo vya ukatili ikiwemo utelekezaji wa watoto.
Na, Josephine Kiravu
Kwenye kampeni ya msaada wa kisheria kwa mkoa wa kigoma, wananchi wamepata nafasi ya kusikilizwa na kupatiwa ushauri kuhusu masuala ya kisheria.
Miongoni mwa mambo yalioibuliwa ni pamoja na migogoro ya ardhi na utelekezaji wa familia ambapo imeelezwa kuwa wazazi vijana kuanzia ambao umri wao ni chini ya miaka 35 wameonekana kuacha uangalizi wa watoto kwa bibi na babu zao hali ambayo inatajwa huenda ikachangia uwepo wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kama anavyotueleza Mwenyekiti wa mtaa wa Kiguhu kata ya nyasha halmashauri ya mji kasulu.
Na hapa baadhi ya wananchi wanaeleza mwarobaini wa tatizo hili la utelekezaji watoto na kutoa ushauri pia kwa wazazi kulea watoto ili kutengeneza kizazi bora chenye maadili yaliyo mema.
Mama Samia legal Aids kwa mkoa wa Kigoma imefanikiwa kutatua na kutoa ushauri kwenye migogoro kadhaa ikiwemo ardhi katika eneo la Kabanda halmashauri ya mji kasulu pamoja na kutoa ushauri kwa wanandoa ambapo pamoja na mambo mengine kwa Kigoma kampeni hii imefikia tamati hapo jana.