Joy FM

TAKUKURU Geita yabaini udanganyifu miradi ya maendeleo

4 February 2025, 09:45

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Geita imebaini mapungufu makubwa kwenye miradi 4 yenye thaani ya shilingi bilioni 1 milioni 45 na laki 6 kati ya miradi 34 yenye thamani ya shilingi bilioni 16.6 iliyofanyiwa ufuatiliaji mkoani humo

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Azza Mtaita ameeleza hayo katika taarifa ya kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, taarifa ambayo ameitoa kwa waandishi wa habari ikiwa ni taarifa ya mwezi oktoba disemba 2024 ambapo amesema miradi hiyo ni kati ya miradi 11 iliyobainika kuwa na mapungufu huku miradi 7 yenye thamani ya sh. 2,719,180,029 ikiwa na mapungufu madogo madogo

Azza Mtaita amesema katika kipindi hicho pia wamefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 1,348,164 ambazo ni matokeo ya udanganyifu uliofanywa na mzabuni Bahati Bundala ambaye alilabidhi nondo zenye kiwango cha chini tofauti na kiwango kilichopo kwenye mkataba katika ujenzi wa shule mpya ya msingi Bwawani wilayani Geita

Amesema nondo ambazo mzabuni huyo alipaswakukabidhi ni nondo zenye kiwango cha ubora wa 460N/MM2 lakini yeye alikabidhi nondo zenye ubora wa 350N/MM2

Kufuatia changamoto hiyo, uongozi wa shule ulishauriwa kumtaka mzabuni huyo kuleta kukabidhi nondo zinazotakiwa

Hata hivyo TAKUKURU mkoa wa Geita imesema inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia TAKUKURU rafiki, mikutano na semina mbalimbali ili kuwajengea wananchi uelewa wa kuripoti matukio ya vitendo vya rushwa